Phoenix Hatua za Kiswahili Rasmi GD4

Hatua za Kiswahili Rasmi, Kitabu cha mwanafunzi ni mfululizo wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa ufundi kwa kufuata _x000D_
mtalaa mpya unaosisitiza umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kukuza weledi wake katika stadi za kusikiliza na _x000D_
kuzungumza, sarufi na matumizi ya lugha, kusoma na kuandika. Vitabu hivi vina sifa zifuatazo: • Mada kuu zilizopangwa kwa _x000D_
kuzingatia ruwaza ya mtalaa ya Kiswahili Gredi ya 4 ili_x000D_
kurahisisha utumiaji. Vipindi vilivyopangwa kushughulikia mada ndogo mbalimbali kulingana na ruwaza ya mtalaa._x000D_
Picha na michoro iliyochorwa kwa rangi za kupendeza ili kuvutia usomaji na ujifunzaji. • Maswali dodoso yanayochochea _x000D_
uwezo wa mwanafunzi kufikiria na kudadisi masuala_x000D_
mbalimbali. Kazi za ziada na majaribio yanayomhusisha mwanafunzi binafsi, wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi kwenye _x000D_
makundi katika shughuli ainąaina. Mradi wa nyumbani unaowahusisha wazazi na walezi katika ujifunzaji wa Kiswahili na pia_x000D_
kukuza uwajibikaji. · Hadithi na utajiri wa shughuli nyingine zinazokuza umilisi wa kimsingi wa lugha ya Kiswahili_x000D_
na zilizooanishwa na masuala mtambuko, maadili chanya miongoni mwa masuala mengine._x000D_
Matumizi ya teknolojia kwa mfano kusikiliza sauti redioni na unasaji sauti kwa kutumia • simu na vifaa vingine vya _x000D_
kiteknolojia. Mathias Momanyi ni mtafiti, mwandishi, mwalimu na mwanahabari mashuhuri. Ameandika vitabu vingi vikiwemo _x000D_
msururu wa Kilele cha Insha vilivyosifiwa kwa ukwasi wake wa fani na tamathali za lugha komavu. Yahya Mutuku ni mwandishi _x000D_
na vilevile mwalimu mwenye uzoefu na utaalamu mkubwa. Ameshiriki kikamilifu katika harakati, na mikakati ya ukuzaji wa _x000D_
Kiswahili kupitia vipindi vya Kiswahili. Ameshirikiana na Mathias Momanyi kuandika msururu wa Kilele cha’ Insha _x000D_
vilivyosifiwa kwa ukwasi wake wa fani na tamathali za lugha komavu. Pia ameandika hadithi nyingi pamoja na Kamusi ya Picha.

KSh 638.00

wws Maya / Pre-sale Questions Need Help? Contact Us via WhatsApp

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Phoenix Hatua za Kiswahili Rasmi GD4”

//
Our customer support team is here to answer your questions. Ask us anything!
👋 Hi, how can I help?