Maisha Kitendawili

“Mahaba ni mithili ya kondo; yakushikapo yanakutia donda. Penzi la Farida kwa Kim limegeuka na kuwa pendo. Farida sasa katota…” Itakuwaje? Riwaya hii ya kusisimua inatuingiza katika bahari tesi ambamo asiyesimama imara huzama ji! Unapoisoma unachukuliwa na wimbi la vitushi vya hadithi iliyotambwa kwa ufundi wa kipekee. Maisha Kitendawili ni riwaya ya pili ya Dkt. John Habwe. Riwaya yake ya kwanza, Maumbile si Huja, imewafurahisha wapenzi wa fasihi ya Kiswahili, si haba. Pia, ameandika hadithi fupi kama vile “Pendo la Heba ” na “Walicheka Kicheko”. Mwandishi amejibainisha kuwa na uketo wa lugha ya Kiswahili na uelewa mpana wa matukio na mitagusano inayopitikia jamii za kisasa. Mwalimu Habwe ni mtaalamu wa Isimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

KSh 514

wws Maya / Pre-sale Questions Need Help? Contact Us via WhatsApp

untitled design 24

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Maisha Kitendawili”

//
Our customer support team is here to answer your questions. Ask us anything!
👋 Hi, how can I help?