Mkuu: Si Kitu
Wote wawili, Sofi na Sali, walikuwa katika nyumba He He wakiwa wamefichwa: mmoja akiitunza siri na kutunzwa kisiri huku mwingine akiteswa kisiri kwa sababu ya siri.Chaanasa anakabiliwa na utata kuhusu maisha yake. Hawafahamu wazazi wake, wala hajui ikiwa bado wanaishi. Anayeijua historia yake naye anaifanya kuwa siri kubwa; siri ambayo anaihifadhi katika moyo – kiungo kidogo tu – ili kumlinda Chaanasa. Je, siri yenyewe inahusu nini kiasi cha kutunzwa, na mtu kuteswa? Je, Chaanasa atafanya juhudi kuibaini au atayaona hayo kuwa si kitu?Shullam Nzioka ni mwandishi chipukizi anayedhihirisha umilisi wake wa lugha ya Kiswahili kupitia hadithi hii iliyosukwa kwa mtindo utakaomvutia msomaji hadi hatima ya kisa chenyewe. Hiki ni kitabu chake cha kwanza kuwahi kuchapishwa.
Reviews
There are no reviews yet.